Posts

Showing posts from August 27, 2015

Tazama Picha za Mafuriko ya Wanawake Waliojitokeza Millenium Tower Kumsikiliza Lowassa, Wengi Wamekosa Nafasi na Kubakia Nje

Image
Ni mkutano wa wanawake wa ukawa na mh lowasa hapa jengo la millenium TOWER Dar es salaam,hizi ni picha za awali,hizi ni picha za awali ambazo nimekuwekea hapa kutoka katika mkutano huo.LOWASA bado hajawasili hapa ila idadi ya wanawake waliojitokeza hapa ni wengi sana kiasi cha kutokutosha katika jengo hili na sasa watu wanasubiri hatma yao kama watahamisha mkutano au italazimu wengine kuwa wapole na kusubiri nje kidogo. Picha kamili za tukio hili zitakujia baadae kadiri muda unavyozidi kwenda msomaji wetu

Baada ya Kufunguliwa Kamati Mpya ya Miss Tanzania yawekwa Wazi..Jokate Ndani....

Image
Baada ya kufunguliwa kwa mashindano ya kumtafuta Miss Tanzania na Baraza la Sanaa la Tanzania (BASATA), Kamati ya Maandalizi ya Michuano hiyo imekuja na mikakati ya kurejesha hadhi na heshima ya mashindano hayo makubwa ya kusaka walimbwende nchini. Katika kuboresha mashindano ya Miss Tanzania, Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino Agency, Hashim Lundenga leo ametambulisha mbele ya waandishi wa habari kamati mpya yenye wajumbe 12, ambayo itakuwa inaratibu mashindayo hayo kwa sasa. Lundenga amesema kuwa kamati hiyo inayoanza kazi zake hii leo, itashughulikia mapungufu yote yaliyojitokeza na kurejesha imani ya wananchi kwa mashindano hayo ikishirikiana kwa karibu na wadau mbalimbali pamoja na Basata. Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutambulishwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Jokate Mwegelo ametoa shukrani kwa niaba ya kamati yake kwa kuamininiwa kupewa jukumu hilo na kuahidi maboresho makubwa na mikakati endelevu ya kurejesha hadhi ya Miss Tanzania. Kamati Mpya ya Miss Tanzania